Waziri mkuu Iraq atangaza ushindi dhidi ya Islamic State

Waziri mkuu wa Iraq Haider al-Abadi amewasili jijini Mosul kuvipongeza vikosi vya Iraq kwa ushindi wao dhidi ya kundi la Islamic State katika mji huo. Taarifa kutoka ofisi yake ilisema Abadi alikuwa katika mji huo kutangaza ukombozi wa mji huo na ushindi.A� Tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita vikosi vya Iraq vikisaidiwa na mashambulizi ya angani ya Marekani viliwafurusha wapiganaji hao kutoka mji huo wa kale. Wanamgambo wa Islamic State waliuteka mji huo hapo Juni mwaka wa 2014 kabla ya kuchukua ardhi waarabu wa kabila la Sunni huko Iraq na kutangaza taifa la kiislamu huko Iraq na Syria. Wapiganaji wa kikundi cha Peshmerga, wale wa kabila la Sunni na wapiganaji wa kabila la Shia walihusika katika mapigano hayo.