Waziri Mkuu David Cameron Atarajiwa Kujadili Athari Ya Kura Ya Maamuzi Katika Kongamano La Jumuiya Ya Ulaya

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron anatarajiwa kukutana na viongozi wa jumuiya ya ulaya kwa mara ya kwanza tangu Uingereza ipige kura ya kujiondoa katika jumuiya ya ulaya. Cameron anatarajiwa kujadili athari za kura hiyo ya maamuzi na kinachotarajiwa katika kongamano la jumuiya ya ulaya linalotarajiwa kuandaliwa jijini Brussels Ubelgiji. Viongozi wa mataifa ya Ujerumani, Ufaransa na Italia walisema jana kuwa hakutakuwa na mazungumzo yoyote kuhusu hatua ya Uingereza ya kujiondoa katika jumuiya ya ulaya katika mkutano huo. Wakati huo huo chansela George Osborne ameondolea uwezekano wa kuchukuwa mahala pa Cameron katika wadhifa wa waziri mkuu wa Uingereza. Haya yanawadia huku waziri anayeshughulikia maswala ya afya nchini Uingereza Jeremy Hunt akisisitiza kuwa Uingereza inapaswa kusalia katika soko la jumuiya ya ulaya. Wakati huo huo wabunge wa chama cha leba leo watapiga kura katika hoja ya kutokuwa na imani na kiongozi wa chama hicho Jeremy Corbyn.