Waziri Mevlut Cavusoglu, Alaumu Muungano Wa Ulaya Kwa Kuhangaisha Nchi Yake

cavusoglu1
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uturuki, Mevlut Cavusoglu amelaumu muungano wa ulaya kwa kuhangaisha nchi yake huku akikariri msimamo wa serikali yake wa kutaka usafiri huru bila hitaji la hati ya visa kwa ubadilishanaji na kuzuia wahamiaji kumiminika barani ulaya.
Waziri huyo kwenye mahojiano alisema raia wa Uturuki walitamaushwa na jaribio la mapinduzi ya serikali lililotibuka tarehe 15 mwezi uliopita. Uhusiano kati ya muungano wa ulaya na Uturuki umezorota tangu wakati wa jaribio hilo la mapinduzi dhidi ya rais Recep Tayyip Erdogan huku bara ulaya likieleza kuto-ridhika na msako uliofuatia.

Uturuki imeghadhabika na kukatalia mbali shtuma hizo za muungano wa ulaya kwamba misako inayotekelezwa huenda ikakiuka viwango vya haki za kibinadamu ambazo sharti Uturuki itekeleze chini ya makubaliano ya kubadilishana na safari huru pasipo viza na pia kuharakisha mashauri kuhusu kuhusu uanachama wa Uturuki katika muungano wa ulaya. Cavusoglu anasema licha ya Uturuki kufanya juhudi za kutimiza masharti hayo nchi hiyo imepokea tu vitisho, matusi na vikwazo kwa ubadilishanaji.