Wazee wa jamii ya Tugen wafutilia mbali mikutano ya amani katika kaunti ya Baringo

Wazee wa jamii ya Tugen katika kaunti yaA� Baringo wamefutilia mbali mikutano ya amani hadi serikali itakapotwaa bunduki zote zinazomilikiwa kinyume cha sheria katika sehemu hiyo.Hatua hiyo inafuatia mauaji ya zaidi ya watu 20 katika kaunti hiyo kwenye mashambulizi kadha ya wahalifu kwenye kipindi cha majuma matatu yaliopita.Akiwahutubia wanahabari mjini Kabarnet ,mwenyekiti wa baraza hilo la wazeeA� Zachariah Chirchir alikashifu mauaji hayo akiongeza kuwa wamefutilia mbali mashauri baina ya jamii za Pokot na Tugen ili kutoa fursa kwa wanajeshi wa KDF kutekeleza oparesheni yao katika sehemu hiyo.Alisema wanajeshi wa KDF wanapaswa kupewa fursa ya kutekeleza kikamilifu operesheni hiyo ya kutwaa bunduki zote haramu na kuwatia nguvuni wahalifu kama walivyoagizwa na raisA� Uhuru Kenyatta katika juhudi za kudumisha amani katika kaunti hiyo. Wazee hao pia waliihimiza serikali kuchukua hatua za haraka kuwapa makao zaidi ya watu 30,000 walioachwa bila makao kufuatia mashambulizi ya wahalifu kutoka jamii ya Pokot katika kaunti ndogo za Baringo kaskazini,kusini na Tiaty.Kudorora kwa usalama katika sehemu hiyo pia kumeathiri vikao vya bunge la Baringo huku waakilishi wa wodi kutoka jamii ya Pokot akiwemo spika wa bunge hilo William Kamket wakikosa kuhudhuria vikao hivyo.Mwakilishi wa wodi wa Ilchamus Wesley Lekakimon alitoa wito kwa wakaazi kuungana na kudumisha amani kwa ajili ya maendeleo katika kaunti hiyo.