Wazee wa Borana na Gada wapendekeza kuchaguliwa tena kwa Wario

Wazee kutoka makabila ya Borana na Gada wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kumchagua tena waziri wa michezo na utamaduni Hassan Wario kwenye baraza lake jipya la mawaziri. Akiongea kwenye mkutano wa wazee hao mjini Moyale,rais wa kabila la Borana Qura Jarso alisema kuwa Wario amekuwa kielelezo kizuri cha amani katika kaunti ya Marsabit alipokuwa waziri wa michezo.Jarso alisisitizia umuhimu wa demokrasia ya mashauriano na kwamba Wario anastahili kuchaguliwa tena kwenye baraza jipya la mawaziri kufwatia rekodi yake nzuri ya maendeleo katika sehemu hiyo.Aidha wazee hao waligusia swala la umoja baina ya wazee wa sehemu hiyo,akisema uhusiano baina ya waziri huo na gavana wa Marsabit Muhamad Ali ni mzuri.Mwenyekiti wa baraza la wazee wa Borana Gorres Waqo alisema kuwa wanachama waandamizi watano kutoka kabila la Gada wameteuliwa ili kuendeleza juhudi za upatanisho na viongozi wengine wa sehemu hiyo.