Wayne Rooney apigwa marufuku kuendesha gari kwa muda wa miaka miwili

Aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney,A� amepigwa marufuku kuendesha gari kwa muda wa miaka miwili na kuamriwa kufanya kazi kwa muda wa saa mia moja bila malipo, baada ya kukiri kwamba aliendesha gari akiwa mlevi. Mshambulizi huyo wa Everton alisimamishwa na polisi wakati alipokuwa akiendesha gari aina ya a�?Volkswagen Beetlea�? ya mwanamke mmojaA� saa nane usiku tarehe mosi mwezi huu, wakati mkewe mjaa mzito na wanaweA� watatu wakiwa likizoni.A� Mahakama ya a�?Stockporta�? iliyoko Kaskazini-Magharibi mwa Uingereza ilifahamishwa kuwa Rooney alikuwa amepitisha mara tatu kiwango cha pombe kinachoruhusiwa kwa dereva yeyote kunywa na kuendesha gari. Rooney alipokelewa kwa taadhima kuu aliporejeaA� uwanjani Old Trafford, Jumapii iliyopita wakatiA� timu yake ya awali Manchester United ilipoishinda timu yake ya sasa Everton mabao manne kwa bila. Everton kwa sasa inashikilia nafasi ya 18 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza, baada ya kushindwa mechi tatuA� mfululizo.