Wavinya Ndeti azuiwa kuwania Ugavana Machakos

Jopo la kusuluhisha mizozo la tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC limemchuja mwaniaji ugavana wa Machakos Wavinya Ndeti. Hili ni pigo kubwa kwa chama cha Wiper baada ya jopo la tume ya IEBC, likiongozwa na mwenyekiti Wafula Chebukati, kumzuia Ndeti kushiriki kwenye kinyanga��anyiro hicho kwa kuwa mwanachama wa vyama viwili wakati mmoja.Jopo hilo lilikubali malalamishi yaliyowasilishwa na mpiga kura A�Kyalo Peter Kyuli, ambaye pia ni mwanachama wa bunge la kaunty ya Machakos la kuitaka tume ya IEBC ifutilie mbali uteuzi wa Ndeti na kumpokonya cheti alichopewa na chama cha Whiper kuwania ugavana wa kaunty ya Machakos.Kwenye ombi lake,Kyalo, anasisitiza kwamba Ndeti amekosa kutimiza masharti kadhaa ya tume ya IEBC ya kuwania wadhifa wa uteuzi.Alidai kwamba Ndeti ni mwanachama wa vyama viwili ambavyo ni Wiper Democratic Movement na Chama Cha Uzalendo (CCU). Ndeti, hatahivyo alipinga madai hayo akisema uteuzi wake ni halali.Alihimiza jopo hilo kupuzuilia mbali malalamishi hayo akisema suala hilo lilikuwa tayari limeshughulikiwa na jopo jingine halali.Ombi hilo la Kyuli liliungwa mkono na seneta wa Machakos , Johnstone Muthama, ambaye pia alitaka uteuzi wa Wavinya na chama chama cha Wiper ufutiliwe mbali.Kwenye taarifa yake Senator Muthama alisisitiza kwamba uteuzi wa Ndeti unaendea kinyume cha sheria za uteuzi wa chama cha Wiper na uchaguzi na vile vile sheria ya vyama vya kisiasa.