Wauguzi watishia kugoma

Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wauguzi Seth Panyako, amezishtumu Kaunti 13 za humu nchini kwa kukosa kutekeleza haraka mkataba wa mwaka 2017 kuhusu kurejea kazini ambao ulitiwa saini tarehe 2 Novemba. Katibu huyo kwa sasa anatishia kushawishi wauguzi kwenye Kaunti hizo 13 kususia kazi. Mgomo huo kulingana na Panyako utaanza tarehe 11 Januari iwapo kufikia wakati huo, Kaunti hizo hazitakuwa zimetekeleza mkataba wa kurejea kazini kama ilivyokubaliwa. Alitaja Kaunti hizo kuwa za Bungoma, Nyeri, Nakuru, Laikipia, Homa Bay, Elgeyo Marakwet, Tharaka Nithi, Makueni, Kakamega, Wajir, Kirinyaga, Muranga��a na Kericho.

Panyako amesema kwamba serikali za Kaunti zilipaswa kuwalipa wauguzi malimbikizi ya pesa zilizozuiliwa wakati wa mgomo wao kabla ya tarehe 31 Disemba mwaka uliopita.

Wauguzi walirejea kazini mnamo tarehe 3A�A�Novemba baada ya serikali kuahidi kuwapa mishahara yao ilioyokluwa ikizuiliwa kufikia tarehe 30 Novemba, baada ya baraza la Magavana nchini, wizara ya afya na chama cha kitaifa cha wauguzi (KNUN) kutia saini mkataba wa makubaliano ya pamoja kuhusu nyongeza ya mishahara yaani (CBA), hivyo kumaliza mgomo wa wauguzi ambao ulidumu siku 151.