Wauguzi wapuuzilia mbali barua ya kutangaza kazi zao wazi

Wauguzi wanaogoma wamepuuzilia mbali barua iliyodaiwa kuandikwa na afisa mkuu wa baraza la Ma-Gavana nchini, Jacqueline Mogeni, akiwaagizaA� ma-Gavana kutangaza kazi zao kuwa wazi. Akihutubia wana-habari nje ya Jumba la Afya House jijini Nairobi baada ya kuongoza maandamano ya amaniA� kutoka uwanja wa Uhuru Park, naibu wa katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha wauguzi Maurice Opetu, alisemaA� kwamba baraza hilo la Ma-Gavana halina mamlaka ya kuwachukulia wauguzi hatua za kinidhamu, kwani hilo ni jukumu la tume ya kuajiri watumishi wa umma. Aidha, aliwaambia Ma-Gavana wadhubutu kutafuta wahudumu wa afya kutoka nje ya taifa hili, akisema wauguzi hawatarejea kazini hadi kutekelezwa kikamilifu kwa mkataba wao wa nyongeza ya mishahara. Mgomo wa wauguzi kwenye hospitali za umma umedumu miezi mitatu sasa huku wakilalama kuhusu malipo duni. Ijumaa iliyopita, afisa huyo mkuu wa baraza la Ma-Gavana nchini aliwaandikia Ma-gavana na kuwahimiza watangaze kuwa wazi, nafasi ya muuguzi yeyote katika maeneo yao ambaye hatakuwa amerejea kazini kufikia tarehe 8 Septemba.