Wauguzi katika hospitali za uma wagoma

Wauguzi katika hospitali za uma wameanza mgomo ili kushinikiza kutiwa saini kwa mkataba wa nyongeza ya mshahara na marupurupu na serikali za kaunty.Kulingana na maafisa wa chama cha kitaifa cha wauguzi nchini (KNUN), mkataba huo ulitiwa saini mapema mwaka huu.Chama hicho pia kinataka mkataba huo uliotiwa saini iwasilishwe katika mahakama ya kushughulikia mizozo ya ajira ili utekelezwe.Uchunguzi katika hospitali mbali mbali za uma umeonyesha kwamba wauguzi wamegoma na wachache waliofika kazini hawatoi huduma zozote.Hospitali ambako huduma zimekwama ni pamoja na Mama Lucy jijini Nairobi, Hospitali kuu ya mkoa wa pwani, Moi teaching and referral Eldoret, Kisii level five na kituo cha afuay cha Matete huko Lugari katika kaunty ya kakamega.Wagonjwa wamelazimika kutafuta huduma kwingineko. Wakati huo huo baraza la magavana leo linatarajiwa kutoa taarifa kuhusu mgomo huo wa wauguzi.baraza hilo linatarajiwa kutangaza msimamo wake kuhusiana na mkataba huo.Akitangaza kuanza kwa mgomo huo jana, kaimu katibu mkuu wa chama cha wauguzi nchini Morris Opetu alisema waliamua kuitisha mgomo huo baada ya serikali za kaunty kukataa kutia saini mkataba nao.