Watu wawili wauwawa katika maandamano nchini Venezuela

Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi nchini Venezuela katika maandamano dhidi ya serikali ya rais wa taifa hilo Nicolas Maduro. Kijana mmoja chipukizi alifariki katika mji mkuu wa taifa hilo A�Caracas huku mwanamke mmoja akiuawa katika eneo la A�San Cristobal karibu na mpaka wa A�Colombia. Maelfu ya watu waliandamana ili kushinikiza uchaguzi mpya wa urais na kuachiliwa huru kwa wanasiasa waliofungwa gerezani. Rais Maduro aliushtumu upinzani kwa kuwashambulia polisi na kupora maduka. Alisema kuwa watu 30 wamekamatwa. Wafuasi wa serikali wanaandaa mkutano wao katika mji huo wa Caracas. Licha ya kuzalisha mafuta kwa wingi ulimwenguni, Venezuela imekumbwa na miaka mingi ya gharama ya juu ya maisha, ongezeko la uhalifu na uhaba wa bidhaa za kimsingi. A�Maandamano yanayofanyika nchini humo yanalenga kumshinikiza rais Maduro kufanya mazungumzo na upinzani ili kutafuta namna ya kutatua mzozo wa kiuchumi nchini humo.