Watu wawili wauwawa katika jumba la burudani nchini Marekani

 Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi kwenye  jumba moja la burudani mjini Jacksonville, jimboni Florida nchini Marekani.Kulingana na polisi  David Katz,mwanamume wa umri wa miaka 24 alijiuwa kwa kujipiga risasi mara tu baada ya kutekeleza mauaji hayo.Hakuna washukiwa wengine wanatafutwa kuhusiana na kisa hicho.

Takriban watu 11 walijeuhiwa kwenye mkasa huo,ambao ulitokea kwenye jumba la mashindano ya tafrija ya video mjini Jacksonville.Jumba hilo pia  lina maduka na migahawa.Polisi hawakutaka kuthibitisha madai kuwa mwanamume huyo alianza kufyatua risasi baada ya kughadhabishwa kwa kushindwa kwenye mchezo huo wa kamari kwa njia ya video.

Jimbo la Florida limeshuhudia msururu wa visa vya mauaji ya aina hiyo mnamo miaka ya hivi majuzi,yakiwemo yale yaliotokea kwenye klabu kimoja mjini Orlando mwaka wa 2016,ambapo watu 49 waliuawa na kisa cha pili kwenye shule ya upili ya Marjory Stoneman Douglas ,mjini Parkland mnamo mezi wa Februari ambapo watu 17 waliuliwa.