Watu Wawili Wafariki Kwenye Ajali Ya Barabara

Watu wawili wamefariki kwenye ajali ya barabarani iliyotokea katika Mto Nithi kaunti ndogo ya Maara. Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi huko Maara John Njihia amesema gari dogo lililokuwa likitoka Chuka kuelekea Chogoria lilipoteza mwelekeo na kubingiria mara kadhaa kabla ya kutumbukia mto huo. Njihia amesema gari hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi kupita kiasi na inashukiwa kuwa dereva na abiria aliyekuwa naye walikuwa wamelewa . Njihia amewaonya madereva dhidi ya uendeshaji magari kwa kasi kupita kiasi. Miili ya waliofariki imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Chuka kusubiri upasuaji.