Watu Wawili Wafariki Kwenye Ajali Ya Barabara

Watu wawili walifariki papo hapo huku wengine watano wakijeruhiwa vibaya wakati gari aina ya Nissan matatu walimokuwa wakisafiria lilipogongana na lori lililokuwa likisafirisha mchanga katika barabara kuu ya Kisumu kuelekea Busia. Kwa mujibu wa kamanda wa polisi huko Vihiga Sara Duncan, matatu hiyo ambayo hutumika kubeba maiti, ilikuwa imetoka kusafirisha maiti hadi katika eneo la Buyangu na ilikuwa ikirejea mjini Kisumu wakati ajali hiyo ilipotokea. Kwa mujibu wa mashahidi, dereva wa matatu hiyo alikuwa akiendesha kwa kasi kupita kiasi kabla ya kupoteza mwelekeo na kugonga lori. Dereva wa matatu hiyo na mmoja wa abiria wake walifariki papo hapo huku dereva wa lori hilo akijeruhiwa vibaya. Majeruhi wanne katika ajali hiyo walilazwa katika hospitali ya Coptic huko Emuhaya. Kamanda huyo wa polisi alisema kuwa eneo ambako ajali hiyo ilitokea huwa hatari huku akiwatahadharisha madereva kuwa waangalifu wanapoendesha magari katika eneo hilo.

A�