Watu watatu wauawa na wengine wanne kujeruhiwa vibaya Baragoi

Watu watatu wameuawa na wengine wanane kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la wahalifu mjini Baragoi kaunti ya Samburu. Kulingana na afisa mkuu wa matibabu katika hospitali ya matibabu maalum ya kaunti hiyo Robert Nato, wawili kati ya majeruhi hao wamelazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta wakiwa katika hali mahututi. Shambulizi hilo lilitekelezwa mwendo wa saa kumi na moja jioni jana katika sehemu ya Suyan na watu wanaoshukiwa kutoka jamii moja jirani. Polisi wamesema maafisa zaidi wa usalama tayari wamepelekwa katika sehemu hiyo.