Watu watatu wafariki kupitia ajali ya treni, Washington

Yamkini watu watatu wamethibitishwa kufariki dunia baada ya treni moja kutoka kwenye njia ya reli na kuanguka katika jimbo la Washington ,nchini Marekani wakati wa asubuhi watu walipokuwa wanakwenda kazini.Zaidi ya manusura 100 walilazwa kwenye hospitali tofauti jimboni humo kutokana na ajali hiyo.Idadi kubwa ya majeruhi waliripotiwa kuwa mahututi.Kwa mujibu wa maafisa wa shirika la reli la nchi hiyo mabehewa yote yamepekuliwa,japo wamesema kuna uwezekano wa idadi ya waliokufa kuongezeka.Takriban magari saba,mawili yayo malori yaligongwa wakati ajali hiyo ilipotokea.Hiyo ilikuwamara ya kwanza kwa trenin hioyo ya kampuni ya Amtrak kupitia njia hiyo mpya,iliyokuwa ikitumiwa na treni za kubebea mizigo ambayo ni fupi.Treni hiyo ilikuwa ikitoka mji wa Seattle ikielekea mji wa Tacoma