Watu Watano Walazwa Katika Hospitali Ya Garissa Kufuatia Kuzuka Kwa Kipindupindu

Watu Watano wamelazwa katika hospitali ya matibabu maalum ya Garissa kufuatia chamuko la ugonjwa wa kipindupindu katika eneo la Boka kaunti ya Tana River. Kwa mujibu wa muuguzi mkuu katika hospitali hiyo, Hassan Abdullahi, watu wanne wako katika hali thabiti na wataruhusiwa kuondoka hospitalini hivi karibuni. Mgonjwa wa tano bado yuko katika hali mbaya. Hassan alisema wagonjwa hao wamefanyiwa uchunguzi wa kina. Afisa mkuu wa maswala ya afya katika sehemu hiyo,A�Ahmed Dhakane amewahimiza wakazi wa Garissa kuchukua hatua za kujikinga kwani ugonjwa huo umeenea kutoka nchi moja jirani.