Watu Wanne Waangamia Na wengine 17 Kujeruhiwa Kwenye Mlipuko Uturuki

Washukiwa wanne wa utengenezaji mabomu waliuawa na watu 17 kujeruhiwa kwenye mlipuko katika kijiji kimoja cha wakurdi, kusini mashriki ya Uturuki, kwa mujibu wa wizara ya maswala ya ndani ya taifa hilo. Mlipuko huo ulitokea saa nne na nusu usiku katika wilaya ya Sarikamis, umbali wa kilomita 25 kutoka mji wa Diyabarkir, wakati wanamgambo wa chama cha PKK walipokuwawakipakia vilipuzi kwenye gari moja dogo.

Huduma za umeme katika mji wa Sarikamis zimekatizwa,huku nyumba kadhaa zilizo karibu na mahala kulipotokea mkasa zikiathirika,kwa mujibu wa ripota wa shirika la A�habari la CNN.Mlipuko huo ulifwatia mwingine kwenye gari dogo karibu na kambi moja ya kijeshi wakati wa mchana viungani mwa mji wa Istanbul na kusababisha majeraha kwa watu 7.Awali kulitokea mlipuko mwingine wa bomu siku ya jumanne katika mji wa Diyabrkir lililolenga maafisa wa polisi na kusababisha vifo vya watu 3.