Watu sita wauwawa katika maandamano Congo

Watu sita wameuawa katika maandamano yanayoendelea kushuhudiaA�A�katika taifa la Jamhuri ya kidemokrasia yaA�A�Congo, kwa mujibu wa duru za umoja wa mataifa. Waandamanaji hao wanamshinikiza raisA�A�Joseph Kabila a��ambaye muda wake wa kuhudumu uliisha zaidi ya mwaka mmoja uliopita kujiuzulu. Polisi walitumia vitozaA�A�machozi kuwatawanya waandamanaji jijini Kinshasa ambapo vikosi vya kudumisha amani vya umoja wa mataifa vimepelekwa. Maandamano kama hayo majuma Matatu yaliyopita yalisababisha vifo vya watu kadhaa. Msemaji wa ujumbe wa umoja wa mataifa nchini humo amesema kuwa watu wapatao 50 walijeruhiwa jana huku wengine wakikamatwa. Maandamano yaliitishwa na kanisa katoliki nchini humo ambalo lilisisitiza kuwa yafanywe kwa njia ya amani.A�A�Utawala nchini humo umepiga maarufuku maandamano hayo.

A�