Watu sita wafariki baada ya mvua kubwa eneo la pwani

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwenye eneo la pwani jana ilisababisha vifo vya watu sita na kuvuruga shughuli za usafiri katika kaunti za Mombasa na Kilifi. Na jinsi mwanahabari wetu Wandago Odongo anavyotuarifu watu wanaoishi kwneye maeneo ambayo hukumbwa mara kwa mara na maporomoko ya tope wameshauriwa kuhamia maeneo salama.