Watu sita wafariki baada ya bomu kulipuka mjini Mogadishu

Watu sita wameuawa na wengine wanne kujeruhiwa wakati bomu lililotegwa ndani ya gari lilipolipuliwa karibu na hoteli moja mjini Mogadishu, Somalia. Kapteni Mohamed Hussein alisema bomu hilo lililipuka karibu na hoteli ya Weheliye kwenye barabara yenye shughuli nyingi ya Maka Almukarramah. Hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulizi hilo. Hata hivyo wanamgambo wa al-Shabaab mara kwa mara huhusishwa na mashambulizi kama hayo licha ya juhudi za kimataifa za kuwatimua wanamgambo hao kutoka nchini Somalia.

A�