Watu Saba Wahofiwa Kufariki Kwenye Ajali Ya barabarani Vihiga

Watu saba wanahofiwa kufariki huku wengine kadhaa wakijeruhiwa baada ya matatu waliyokuwa wakisafiria kuhusika katika ajali kwenye barabara ya Kapsabet -Mbale karibu na mto  Wamasavu kaunti ya  Vihiga .  Kulingana na afisa mkuu wa polisi katika eneo hilo  Gilbert Ekirapa dereva wa matatu hiyo yenye nafasi ya abiria 14 alikuwa akijaribu kukwepa kuwagonga waimbaji waliokuwa wakisimama karibu na mto huo ambapo alipoteza mwelekeo na kugonga lori. Mwanachama wa bunge la kaunti anayewakilisha wodi ya Shiru Nixon Butia ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliofika katika eneo la ajali hiyo amesema polisi waliharakisha kuwapeleka waliojeruhiwa  hopsitalini .

Waliojeruhiwa wamelazwa katika hospitali ya misheni ya  Kaimosi huku miili ya waliofariki ikipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya utoaji matibabu maalum ya  Vihiga/ Mbale kaunti ya  Vihiga.