Watu Saba Wafariki Kwenye Ajali Nakuru

Watu saba walifariki jana usiku kwenye ajali ya barabara karibu na daraja ya Ngata, kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret. Polisi wamesema ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa nne unusu usiku ,baada ya trela moja kupoteza mwelekeo na kugonga matatu ya kampuni ya North Rift iliyokuwa ikielekea Eldoret.Watu wengine sita walijeruhiwa vibaya na wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kuu ya Nakuru .Manusura kutoka trela hiyo ambaye hakutaja jina lake kutajwa,alidai kuwa dereva wa trela hilo alikuwa mgonjwa na alikuwa amemeza dawa .Madereva wa magari hayo mawili ni miongoni mwa waliofariki papo hapo .Mapema katika eneo hilo hilo ,basi moja dogo iligonga gari moja la binafsi katika sehemu ya Greensteads, na kuwaua watu wawili papo hapo.Miili ya waliofariki ilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya kaunti ya Nakuru .