Watu Kadhaa Wajeruhiwa Kisumu Kufuatia Maandamano Dhidi Ya IEBC

Watu kadhaa walijeruhiwa leo huko Kisumu wakati maafisa wa polisi walipowatawanya wafuasi wa Cord waliokuwa wakiandamana dhidi ya tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC. Baadhi ya wabunge wa kaunti hiyo wakiongozwa na Shakeel Shabir na vijana walikimbilia usalama wao huku maafisa wa polisi wakiwarushia vitoza machozi. Waandamanaji hao walikusanyika katika eneo la Kondele kabla ya kuelekea katika barabara kuu ya Jomo Kenyatta na ile ya Oginga Odinga. Hatimaye walijaribu kuvamia afisi za IEBC huko Kisumu ili kuwasilisha takwa lao. Hali hiyo A�iliwakanganya watu ambao walipatwa bila kutarajia. Kiongozi wa upinzani A�Raila Odinga amesema hatua ya asasi husika za serikali ya kutochukua hatua kuhusiana na malalamishi A�dhidi ya tume ya IEBC, ni mojawapo wa sababu zilizochochea maandamano hayo. Raila alisema hatua ya serikali ya Jubilee ya kudhibiti bunge la taifa, na kutoshtakiwa kwa makamishna wa tume hiyo ya uchaguzi kuhusiana na ufisadi, kuwa sababu ya upinzani kuandaa maandamano ili kuwaondoa makamishna hao mamlakani.A� A�