Watu kadhaa wahofiwa kufariki kufwatia shambulizi dhidi ya uwanja wa ndege wa kivita wa Tiyas nchini Syria

Watu kadhaa wanahofiwa wamefariki kufwatia shambulizi la dhidi ya uwanja wa ndege za kivita wa Tiyas nchini Syria .Awali serikali ya Syria ilidai kuwa kuna uwezekano wa kuhusika kwa nchi za magharibi,huku kukiwa na madai ya matumizi ya silaha za kemikali dhidi ya maeneo yanayothibitiwa na waasi. A�Marekani na Ufaransa A�zilikuwa zimetisha kuingilia kati ikiwa silaha za kemikali zitatumika,ingawaje zimekanusha kuhusika na shambulizi A�hilo la hivi punde.Rais wa Marekani Donald Trump alionya kuwa kutakuwa gharama kubwa ya kulipa baada ya shambulizi la kemikali katika eneo la Douma,karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Damascus