Watu 80 wafariki kwenye mlipuko wa bomu nchini Afghanistan

Bomu lililipuka karibu na ubalozi wa Ujerumani mjini Kabul, Afghanistan na kusababisha vifo vya watu-80 huku wngine-350 wakijeruhiwa. Inasemekana kuwa wengi wa wahanga wa mlipuko huo uliotokea katika eneo la Zanbaq ni raia. Hakuna kundi lililodai kutekeleza shambulizi hilo lakini makundi ya Taliban na Islamic State yamehusika katika mashambulizi ya hivi majuzi. Wizara ya afya imesema idadi ya majeruhi inatarajiwa kuongezeka. Kuna wanajeshi-8,400 wa marekani nchini Afghanistan pamoja na wengine elf-5 wa shirika la kujihami la NATO. Rais Donald Trump amekuwa akishinikizwa kuongeza idadi ya wanajeshi wa Marekani huko Afghanistan ili kudhibiti harakati za kundi la Taliban ambalo limetwaa zaidi ya thuluthi moja ya nchi ya Afghanistan.