Watu 8 wafariki kwenye ajali ya barabara Timboroa

Watu wanane wamefariki leo asubuhi na wengine-25 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi na lori katika eneo la Hill Tea karibu na Timboroa kwenye barabara kuu ya Eldoret a�� Nakuru. Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Eldama Ravine Agnes Kamau, amesema ajali hiyo ilihusisha basi la kampuni ya Crown lililokuwa likielekea Kakamega na lori. Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya matibabu maalum ya Moi mjini Eldoret na hospitali nyingine mjini humo. Shughuli za uokoaji zinaendelea. Ajali hiyo imejiri baada ya halmashauri ya kitaifa ya usalama na uchukuzi barabarani-NTSA kubuni kanuni mpya za uchukuzi ili kuzuia visa vya uendeshaji magari kwa kasi katika barabara za humu nchini hasa katika maeneo yanayoshuhudia ajali mara kwa mara.