Watu 77 wafariki kwenye ajali Afrika ya kati

Yamkini watu 77 wamefariki baada ya Lori moja lililosheheni abiria na mizigo kuanguka huko jamhuri ya Afrika ya kati. Maafisa wanasema watu wengine kadhaa walijeruhiwa kwenye ajali hiyo karibu na mji wa Bambari, kilomita 300 kutoka mji mkuu Bangui. Wahasiriwa wengi wanasemekana kuwa wafanyibiashara waliokuwa wakielekea kwenye soko moja lililo karibu.

Mara kwa mara, raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati husafiri kwa ma-Lori kutokana na ukosefu wa huduma nyingine za uchukuzi nchini humo.

Chanzo cha ajali hiyo bado kinachunguzwa. Hata hivyo Mbunge mmoja nchini humo amesema Lori hilo lilikuwa likiendeshwa kwa kasi zaidi. Aidha, inahofiwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka. Taifa hilo masikini lisilo na ufuo wa bahari limeghubikwa na mizozo ya kidini na kikabilaA� tangu mwakaA� 2013.