Watu 7 wauawa nchini Mali kufuatia uvamizi

Wavamizi wameshambulia ngome ya kudumisha amani ya umoja wa mataifa ya (UN) katika mji wa kaskazini mwa Mali wa Timbuktu jana na kuwaua watu saba wakiwemo walinzi watano wa Mali na raia mmoja. Hatibu wa ujumbe huo wa umoja wa mataifa Radhia Achouri alisema kuwa kikosi maalum cha kujibu mashambulizi kimetumwa katika eneo hilo.A� Hatibu wa jeshi la Mali Selon Diaran Kone alisema kuwa kisa hicho kimedhibitiwa na wavamizi wanne wakauawa.