Watu 55 Waachiliwa Baada Ya Kutangazwa Kwa Kutokuwepo Kwa Maradhi Ya Ebola

Sierra Leone amewaruhusu watu 55 kuwa huru kusafiri baada ya kutangazwa kuwa wako huru kutokana na ugonjwa wa Ebola. Watu kadhaa walipigwa marufuku kusafiri mwezi uliopita baada ya matukio mawili mapya ya virusi vya ugonjwa huo kuthibitishwa. Msemaji wa huduma za dharura za afya Sidi Yahya Tunis, huko Sierra Leone alisema walioruhusiwa kuwa huru kusafiri walithibitishwa kuwa huru na shirika la afya duniani WHO. Tunis alisema watu wa Sierra Leone wanapaswa kuhakikishiwa kwamba nchi hiyo sasa ina uwezo wa kuudhibiti ugonjwa huo wa Ebola.