Watu 53 wafariki kutokana na moto mkubwa katika mji wa Kemerovo

Takriban watu 53 wamethibitishwa kufariki baada ya moto kuzuka katika jumba moja kubwa la biashara katika mji wa Kemerovo, eneo la Siberia nchini urusi.Kulingana na maafisa nchini humo wanasema watoto 41A� ni miongoni mwa wanaohofiwa kuangamia ,huku watu wengine 16 wakiwa hawajulikani waliko. Moto huo ulianzia ghorofa ya juu ya jumba hilo kwa jina Winter Cherry,ambapo yasemekana wengi wa waliofariki walikuwa kwenye kumbi za sinema wakati moto huo ulipoanza.Kilichosababisha hoto huo hakijabainika lakini uchunguzi unaendelea.Zaidi ya maafisa 600 wamepelekwa katika eneo hilo kusaidia katika shughuli ya uokoaji.