Watu 5 wauawa Guinea katika maandamano ya walimu

Watu watano wameuwa katika mji mkuu wa Guinea ,Conakry kutokana na ghasia na maaandamano ya walimu wanaopinga  sera za serikali kuhusu sheria zinazowahusu wafanyakazi. Hatibu wa serikali  Damatasng Albert Camara  hatimaye alitia saini mwafaka wa kukomesha mgomo huo na kuwaahidi serikali itashughulikia malalamishi yao.Migomo ya kitaifa imekuwa jambo la kawaida nchini humo kwa takriban miaka 10 iliopita.