Watu 40 wameuawa na wengine kujeruhiwa kwenye mlipuko, jijini Kabul

Takriban watu 40 wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa kwenye mlipuko jijini Kabul karibu na afisi za shirika moja la habari na kituo cha kitamaduni kwa mujibu wa wizara ya maswala yakitaifa nchini Afghanistan. Mlipuko huo uliotokea mapema leo ulikumba eneo lililo karibu na shirika la habari la Voice na kituo cha kitamaduni cha Tebyan kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo. Manusura mmoja alisema kuwa wanaharakari walikuwa wamekusanyika katika kituo cha kijamii na kitamaduni cha Tebyan kwa mkutano wakati mlipuaji bomu wa kujitoa mhanga kufa alipolipua vilipuzi vyake. Kamati kuhusu usalama wa wanahabari nchini Afghanistan imeshtumu shambulizi hilo. Hivi maajuzi kamati hiyo iliripoti ongezeko la mashambulizi dhidi ya wanahabari huku yamkini visa 73 vikirekodiwa mwaka huu hili likwa ongezeko la asilimia 35 ikilinganishwa na mwaka uliopita. Mnamo mwezi Mei kundi la wanamgambo la Islamic State lilidai kutekeleza shambulizi dhidi ya jengo la kituo cha running cha kiserikali huko Jalalabad ambapo watu sita waliuawa.