Watu 4 Wauawa Kwa Kugongwa Na Lori Huko Jerusalem

Watu wanne wameuawa huko Jerusalem baada ya mwanaume mmoja raia wa Palestina kuendesha lori na kugonga kundi la  wanajeshi katika kile polisi wanadai kuwa shambulizi la kigaidi.  Wanawake watatu na mwanaume mmoja wa umri wa miaka ishirini waliuawa na wengine 17 kujeruhiwa kwa mujibu wa polisi.  Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema kuwa mvamizi huyo aliuawa baada ya kupigwa risasi na wanajeshi. Inashukiwa kuwa  mvamizi huyo alikuwa mfuasi wa kundi la Islamic State. Hata hivyo waziri huyo mkuu hakutoa ushahidi wa kuunga mkono madai hayo. Waathiriwa walikuwa katika ziara ya kimafunzo kwa mujibu wa jeshi la Israel. Mvamizi  huyo ambaye alitambuliwa  kama Fadi Qunbar mwenye umri wa miaka  28 na  anasemekana kutoka katika jimbo la Jabel Mukaber mashariki ya  Jerusalem.