Watu 37 watiwa nguvuni Paris baada ya ghasia kuzuka

Watu 37 wametiwa nguvuniA� viungani mwa jiji la Paris huko Ufaransa baada ya kuzuka ghasia kufwatia madai ya kudhulumiwa kimapenzi kwa kijana mmoja mweusi na afisa wa polisi akitumia kirungu chake.Takriban watu 2,000 waliandamana nje ya mahakama moja wakitaka haki itekelezwe kuhusu Theo,mwenye umri wa miaka 22 ambaye ilibidi afanyiwe upasuaji mdogo baada ya kutiwa nguvuni kwenye viunga vya mji wa Aulnay-sous-Bois.JapoA� maandamano hayo yalikuwa ya amani,baadaye baadhi ya waandamanaji walikabiliana na polisi walipoanza kushambulia magari na kupora maduka,huku wakiiba mali ya umma.Magari kadhaa na basi moja yaliteketezwa kwenyeA� mtafaruku huo,hjuku vioo vya maduka kadhaa vikivunjwa katika viunga vya mji ulio jirani wa Bobiny.