Watu 35 wafariki kutokana na kipindupindu Nigeria

Watu-35 wamethibitishwa kufariki tangu kuzuka kwa ugonjwa wa kipindu pindu Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kwa mujibu wa maafisa wa afya, ugonjwa huo ulizuka katika kambi yaA�Muna Garage iliyoko katika mji mkuu wa jimbo la Borno, Maiduguri ambako kuna watu elf-20 waliotoroka mashambulizi ya kundi la Boko Haram. Jumla ya visa elf-775 vya ugonjwa wa kipindu pindu vimeripotiwa katika kambi hiyo. Chamuko la ugonjwa huo limechochewa na mazingira mabovu katika kambi hiyo hususan wakati huu wa msimu wa mvua. Hata hivyo, mashirika ya kutoa misaada nchini Nigeria na wale wa kimataifa yanatoa mahema, chakula, maji safi na pia huduma za matibabu kwa wakimbizi hao kwa minajili ya kudhibiti ugonjwa huo.