Watu 34 wauwawa kwenye mlipuko wa bomu mji wa Mogadishu

Yamkini watu 34 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu uliotokea kwenye gari moja katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu.Mkasa huo ulitokea kusini mwa eneo la Madina,kwa mujibu waripoti rasmi.Mlipuko huo ambao uliharibu maduka na vibanda vya kuuzia vyakula ulikuwa shambulio kubwa zaidi kuwahi kutekelezwa A�katika mji wa Mogadishu tangu kuapishwa kwa A�rais Mohamed Abdulahi Mohamed kuwa rais wa nchi hiyo mapema mwezi huu.Hapana kundi lolote limedai kutekeleza shambulizi hilo,japo inadaiwa kuwa huenda A�kundi la Al Shabaab lilitekeleza shambulio hilo.Siku ya jumamosi,kiongozi mwandamizi katika kundi hilo aliapa kuwalenga wafwasi wa rais huyo mpya.