Watu 194 wafariki kwenye mafuriko nchini Sri Lanka

Serikali ya Sri Lanka imetoa wito kwa wafanyikazi wa kujitolea kusaidia katika shughuli za uokoaji kufuatia mafuriko makubwa ambayo hayajawahi kukumba taifa hilo katika kipindi cha miaka-14. Watu-194 wameripotiwa kufariki huku maelfu ya wengine wakiachwa bila makazi. Raia wametakiwa kutoa maji safi ya kunywa baada ya visima vya maji kuharibiwa na mafuriko hayo. Maafisa wa matibabu wanafanya kila juhudi kuzuia chamuko la maradhi ya kipindu pindu nchini humo.