Watu 18 washukiwa kuambukizwa kipindupindu huko Tana Kaskazini

Watu 18 wanapokea matibabu kutokana na maambukizi ya maradhi yanayoshukiwa kuwa kipindupindu katika eneo la Tana Kaskazini, kaunti ya Tana River. A�Mkurugenzi wa Afya katika kaunti hiyo Dkt. Oscar Endekwa, amesema visa vya maambukizi hayo viliripotiwa katika maeneo ya Bura, Bilbil, Anole, Madogo na Matagala. A�Dkt. Endekwa A�alisema sehemu hiyo A�imekumbwa na maradhi hayo kutokana na hali duni ya usafi miongoni mwa wakazi A�na hali kadhalika ukosefu wa maji safi. Alisema maafisa wa afya wamepelekwa sehemu hiyo na wanatoa matibabu pamoja na mafunzo kuhusu usafi kwa wakazi. Hoteli pia zimeamuriwa kufungwa ili kukabiliana na maambukizi ya maradhi hayo. Mwaka uliopita maradhi hayo yalizuka kwenye kambi ya Huduma ya Vijana kwa Taifa ya Bura na kusababisha maafisa 20 kulazwa hospitalini. Idadi kubwa ya wakazi wa sehemu hiyo hawana vyoo.