Watu 16 Wauwawa Nchini Ivory Coast Na Wanamgambo Wa Al Qaeda

Wanamgambo wa tawi la Afrika Kaskazini la mtandao wa al Qaeda wamewaua watu-16 wakiwemo wazungu wanne katika eneo la ufuoni la Grand Bassam nchini Ivory Coast. Wanamgambo sita waliwamiminia risasi watu waliokuwa katika ufuo huo ambao ni maarufu kwa watalii kutoka nchi za Ulaya, umbali wa kilomita-40 Mashariki mwa Abidjan. Waziri wa maswala la ndani wa Ivory Coast, Hamed Bakayoko alisema watalii hao kutoka Ufaransa, Ujerumani, Burkina Faso, Mali na Cameroon ni miongoni mwa watu waliouawa. Walioshuhudia kisa hichio walisema wanamgambo hao walipenya ufuoni humo na kuwamiminia risasi watalii hao kabla ya kushambulia watu waliokuwa kwenye mankuli ya mchana. Serikali imesema wanamgambo hao waliuawa baadaye kwenye makabiliano na maafisa wa usalama.