Watu 14 wauawa Sudan Kusini

Wavamizi nchini Sudan kusini walivamia msafara wa magari uliokuwa ukitoka nchini Uganda ukielekea jijini Juba na kusababisha vifo vya watu 14 wakiwemo wanajeshi kadhaa, kwa mujibu wa hatibu mmoja wa polisi. Msemaji wa jeshi alidhibitisha idadi ya waliouawa na kuongeza kuwa wanajeshi wengine tisa walijeruhiwa. Aliliambia shirika la habari la BBC kuwa baadhi ya majeruhi wanatibiwa jijini Juba. Barabara ya kutoka mpaka wa Uganda kuelekea Juba ni muhimu kwa taifa la A�Sudan kusini.