Watu 13 Wafariki Na Wengine Wengi Kujeruhiwa Katika Milipuko Nchini Ubelgiji

Watu 13 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa katika milipuko miwili ambayo imetokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem mjini Brussels leo asubuhi. Serikali ya Ubelgiji imethibitisha tukio hilo ijapokuwa haijatoa idadi kamili ya waathiriwa.

Watu wameondolewa kutoka kwenye uwanja huo na safari za ndege kutua au kupaa katika uwanja huo kukatizwa.

Vyombo vya habari nchini humo vimesema milipuko hiyoA� ilitokea karibu na meza ya shirika la ndege la American Airlines na kuongeza kua takriban watu 35 wamejeruhiwa vibaya licha ya wengine kufariki.

Haijabainika ni nini chanzo cha milipuko hiyo.

Milipuko pia imeripotiwa katika kituo cha treni cha Maelbeek karibu na majengo taasisi za Umoja wa Ulaya. Mfumo wa uchukuzi wa treni mjini Brussels umefungwa.