Watu 12 wafariki na wengine wanne wajeruhiwa kufuatia moto Bronx

Watu 12 wamefariki na wengine wanne kujeruhiwa vibaya baada ya moto kuzuka katika jumba moja la ghorofa katika eneo la Bronx borough ,huko New York,Marekani .Kulingana na meya wa jiji la New York City Bill de Blasio,mkasa huo wa mto ,ndiyo mbaya zaidi kukumba jiji hilo katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.Amesema miongoni mwa waliofariki ni mtoto wa mwaka moja. Kilichosababisha moto huo hadi sasa hakijabainika.Jumba hilo linapakana na chuo kiku cha Fordham na bustani ya wanyama Bronx. Moto huo ulizimwa baada ya kazi ngumu iliyohusisha zaidi ya wafanyakazi 160 kutoka idara ya kuzima moto.