Watoto wawili wafariki baada ya moto kuzuka katika mtaa wa mabanda wa mukuru jijini Nairobi

Watoto wawili walichomeka hadi kufa jana usiku huku mwingine akiendelea kuuguza majeraha katika hospitali moja humu jijini baada ya moto kuzuka katika mtaa wa mabanda wa Mukuru jijini Nairobi. Wavulana hao wa kati ya umri wa miaka miwili na matatu mtawalio wanasemekana kuachwa na mama yao katika nyumba. Wanasemekana kuchomeka na moto uliosababishwa na msumaa katika eneo la Tetrapark. Dada ya wavulana hao wawili amelazwa hospitalini. Kwa mujibu ya majirani, msumaa huo ulianguka katika kitanda ambapo wawili hao walikuwa wamelala. Juhudi za kuwaokoa ziliambulia patupu. Maiti za wawili hao zilipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City. A�Mapema mwaka huu watu kadhaa walijeruhiwa baada ya moto kuzuka katika mtaa wa mabanda wa Mukuru ambapo shughuli za uokoaji hutatizika kutokana na kurundikana kwa nyumba.