Watatu wanaohusishwa na wizi wa shilingi milioni 50 waachiliwa kwa dhamana

Kwingineko wanaume watatu wanaohusishwa na ule wizi wa shilingi milioni 50 kutoka kwa tawi la Thika la benki ya Kenya Comercial wameachiliwa kwa dhamana.Halford Munene Murakaru mwanawe Charles Mwangi Murakaru na rafiki yao Julius Ndungu Wainaina,waliachiliwa kwa thamana ya shillingi milioni nne kila mmoja na mdhamini wa kiasi kama hicho na hakimu wa Thika Teresia Murigi.mahakama hiyo ilipinga ombi la polisi la kuwataka washtakiwa hao watatu wazuiliwe kwa muda zaidi. Polisi walishindwa kutoa ushahidi wa kuunga mkono ombi lao.Washukiwa hao walikamatwa katika mtaa wa Joyland huko Thika mwishoni mwa wiki ambapo pia walipatikana na shilingi milioni 17.1 katika nyumba moja.Washukiwa hao watatu wakiwa na wengine ambao bado hawajakamatwa wanakabiliwa na shtaka la kuiba shillingi milioni 52 kutoka benki hiyo.Kesi hiyo itatajwa tarehe 14 mwezi desemba A�na kusikizwa kuanzia tarehe 29 mwezi Machi mwaka ujao.