Watano wauwawa na wengine kujeruhiwa kwenye ajali Murang’a

Watu watano wamefariki na wengine tisa kujeruhiwa vibaya kwenye ajali ya barabarani iliyotokea huko Sagana, kaunti ya Murang’a . Ajali hiyo ilihusisha lori lililokuwa likisafirisha mbao A�na matatu mbili jana usiku katika eneo hatari la Mlima Swara karibu na shamba la A�Kakuzi kwenye barabara kuu ya A�Nairobi-Nyeri . Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Makuyu Paul Wanjama amesema lori hilo la kampuni ya Kakuzi Limited lilipoteza mwelekeo na kugonga matatu mbili. Amesema wanawake wanne na mwanamme mmoja walifariki papo hapo . Waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali ya Thika Level 5 . Wanjama amesema matatu hizo mbili ambazo moja ni ya chama cha wenye matatu cha A�Ketno na nyingine ya chama cha A�Emuki zilikuwa zikielekea A�Embu kutoka A�Nairobi wakati ajali hiyo ilipotokea. Vifuzi vya matatu hizo vilikokotwa hadi katika kituo cha polisi cha Makuyu.