Watalii Wanaoeneza Filamu Za Mahaba Waonywa

Halmashauri ya kuorodhesha filamu hapa nchini imewaonya watalii wanaozuru nchi hii dhidi ya kuandaa filamu za mahaba na wasichana wa umri wa mdogo.Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ezekiel Mutua A�amesema halmashauri hiyo A�kwa sasa inashirikiana na polisi A�na makamishna wa kaunti A�katika eneo la Pwani, ambapo utalii wa mahaba unazidi kuongezeka ,ili kuwakamata na kuwashtaki wahusika.Mutua amesema halmashauri hiyo imeanzisha uchunguzi kuhusiana na filamu za ngono kati ya wanawake na mbwa, zinazodaiwa kuandaliwa katika majumba ya kitalii ya kibinafsi katika kaunti ya Mombasa, akionya kwamba watakaopatikana na hatia watachukuliwa hatua kali za kisheria. Akiongea huko Mombasa,Mutua alisema serikali haitawavumulia watalii wanaozuru nchi hii wakiwa nia ya kuharibu maisha ya wasichana wadogo, na pia kujihusisha katika matendo yanayokiuka maadili msingi ya Kiafrika. Aidha alisema halmashauri hiyo imeanzisha utaratibu wa kuiwezesha kufwatilia kila hatua ya maandilizi ya filamu zinazotayarishiwa hapa nchini,ili kuhakikisha kuwa kanuni na masharti A�yote yaliowekwa yanazingatiwa.Aliongeza kwamba halmashauri hiyo imeanzisha ushirikiano na kampuni ya teknolojia ya Google kupitia programu kwa jina Web Rangers,ili kuwawezesha wazazi kuthibiti picha watoto wao wanatazama kupitia mtandao.