Watafiti wa elimu waibua wasiwasi kutokana na ujuzi wa taasisi mbalimbali

Watafiti katika sekta ya elimu wameibua wasi wasi kutokana na kiwango cha ujuzi A�wa A�wanafunzi wanaohitimu kutoka taasisi za mafunzo na kutafuta kazi huku serikali ikiwekeza pakubwa katika sekta hiyo. Kulingana na watafiti hao kutoka A�wadau mbali mbali wakuu katika sekta ya elimu, faida ya uwekezaji huo ni ya kiwango cha chini kuliko inavyotarajiwa na wameshinikiza kutekelezwa kwa mipango ya kuwezesha wanafunzi kupata A�ujuzi unaohitajika . A�Dr. Benjamin Piper kutoka taasisi ya utafiti ya (RTI), amesema licha ya serikali kuwekeza rasil mali nyingi katika sekta ya elimu ikilinganishwa na nchi nyingine jirani , kiwango cha ubora wa elimu ungali chini. Akiongea mjini Nyeri wakati wa warsha ya siku mbili ya kujadili jinsi ya kuboresha masomo hapa nchini, Piper alisema ipo haja ya uwekezaji katika mipango ya kuwapa wanafunzi ujuzi unaohitajika. Hata hivyo watafiti hao wamesema mtaala mpya wa elimu ambao umebuniwa na taasisi ya kuratibu mitaala hapa nchini ambao unatarajiwa kutekelezwa hivi karibuni unaashiria matumaini ya kuleta mageuzi katika sekta ya elimu hapa nchini.