Wasimamimizi Wa Chuo Kikuu Cha Nairobi Watahadhirisha Dhidi Ya Kuingilia Kati Uchaguzi Wa Viongozi

Tume ya uchaguzi katika chuo kikuu cha Nairobi imetahadharisha wasimamizi wa chuo hicho dhidi ya kuingilia kati uchaguzi wa viongozi wa wanafunzi katika chuo hicho.

Tume hiyo inasema haitashawishika katika azma yake ya kuandaa uchaguzi huru na wa haki.

Mwenyekiti wa tume hiyo Avida Zebedie alisema ni ukiukaji wa haki za kimsingi kwa chuo hicho kuwaruhusu wawaniaji ambao hawajahitimu kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Sheria mpya za chama cha wanafunzi wa chuo hicho SONU zinawazuia wawaniaji watakaochukua karatasi zao za uchaguzi siku 19 kabla ya uchaguzi huo kushiriki kwenye kinyanga��anyiro hicho.

Hali kadhalika tume hiyo imezindua mijadala ya umma itakayowahusisha wawaniaji wote.

Na ili kupunguza ghasia kabla ya uchaguzi huo, tume hiyo imesema itatoa hamasisho kwa wanafunzi wote ili kuwawezesha kushiriki kwenye uchaguzi huo kwa njia ya amani.

Uchaguzi wa viongozi wa chama cha SONU umepangiwa kufanyika tarehe mosi mwezi Aprili.