Wasichana watwaa nafasi sita bora za kwanza kwenye mitihani wa KCSE

Wasichana wameendelea kushamiri kwenye mitihani ya taifa na kutwaa nafasi sita bora za kwanza kwenye mtihani wa mwaka huu wa kidato cha nne-KCSE. Naomi Karimi Kawira wa shule ya upili ya wasichana ya Pangani aliibuka mwanafunzi bora zaidi kwa alama 87.01 za wastani, akifuatiwa na Sharon Chepchumba wa shule ya upili ya wasichana ya Moi, Eldoret ambaye alishikilia nafasi ya pili kwa alama 86.83. Sita kati ya wanafunzi bora kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka huu ni wasichana. Mwaka huu wavulana waliweza tu kupata nafasi nne kati ya nafasi kumi bora. Kamau Brian Maina wa shule ya upili ya wavulana ya Alliance alishikilia nafasi ya tatu kwa alama 87.75. Odero Donatta wa shule ya upili ya wavulana ya Alliance alichukua nafasi ya nne, akifuatiwa na Harriet Mueke wa shule ya Mary Hill, Brian Ongiri Okundi, Moraa Monga��ina, Emily Mwatate na Wahome Wanjiku wa shule ya upili ya wasichana wa Moi, Eldoret. Jumla ya watahiniwa 615,773 walifanya mtihani wa mwaka huu ikilinganishwa na watahiniwa 577,253 mwaka uliopita.